Posts

ANGALIA PICHA MTOTO MWINGINE AFANYIWA UKATILI WA KUTISHA NA MAMA YAKE MKUBWA MORO

Image
                           M toto Mwajuma Athuman[6] aliyeokotwa na wanajeshi kambi baada ya kukimbia mateso ukatili anaodai kufanyiwa na mama yake mkubwa Bi,Ashura Omar amefichua siri nzito mbele ya Afisa mtendaji wa kata ya Kingolwira                                                    Mwenyekiti wa Mtaa Tank la Maji  ka ta ya  Kingolwira Bw Mohamed Said akiwa na mtoto huyo Mtoto huyo akiwa na Makovu aliyodai yametokana na kipigo toka kwa mama yake mkubwa Mtoto huyo hawezi kutembea baada ya mguu wa kushoto uliokuwa na kidonda kuvimba,akidai kidonda hicho pia kimetokana na kichapo toka kwa mama yake huyo. Mwenyeki  akimbeba mtoto huyo kueleka ofisi ya Afisa Mtendaji Mama mkubwa wa mtoto huyo baada ya kuona kamera za Mtandao huu zikimmulika alificha sura yake kwa kuinama Afisa Mtendaji wa kata hiyo Bw Rubeni Ndimbo[kulia] akimhoji mama huyo aliyeficha sura yake;aliyevaa nguo za kitenge ni Afisa Mtendaji wa mtaa wa Tenk la Maji Bi,lnocencia Mbena Patri

AVEVA NDIYE RAIS MPYA SIMBA SC...ASHINDA KWA KISHINDO KIKUBWA

Image
Amin Bakhresa  akitangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Simba SC. Evance Aveva akishukuru baada ya kutangazwa kuwa Rais mpya wa klabu ya Simba na kuchukua mikoba ya Ismail Aden Rage, aliyemaliza muda wake wa miaka minne. Rais mpya wa Simba, Aveva akipongeza Bakhresa kwa kazi nzuri ya kusimamia shughuli nzima ya uchaguzi, ambao ulifanyika pasipo bugudha yoyote ile katika Bwalo la Polisi Oysterbay jana  MIKAKATI IMEANZA! Rais mpya wa Simba Aveva (mwenye suti, kushoto), akisalimiana na Katibu Mkuu wa klabu hiyo Ezekiel Kamwaga huku Makamu Katibu Mkuu Phillip Stanley (mwenye shati jekundu) akiwasikiliza mipango yao.   Rais Aveva, akifurahia jambo na Makamu Mwenyekiti uongozi uliomaliza muda wake, Joseph Itang'are 'Mzee Kines' baada ya shughuli nzima ya uchaguzi kumalizika kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi Oysterbay. (PICHA NA RICHARD BUKOS/GPL)

ANGALIA PICHA ALICHOFANYIWA BABA MWENYE NYUMBA HATOSAHAU MAISHANI.

Image
  Jamaa aliyetajwa kwa jina moja la Lugali  akihusishwa  kuchepuka na mke wa mpangaji wake, akiwa amenaswa kwenye gesti moja maeneo ya Buguruni, Dar. Vunja jungu! Saa kadhaa kabla ya kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, jamaa aliyetajwa kwa jina moja la Lugali ameibua sekeseke kwenye nyumba ya kulala wageni (gesti), kisa kikidaiwa ni mchepuko akihusishwa na mke wa mpangaji wake, Ijumaa Wikienda lina kisa na mkasa. Wakati ikirandaranda mitaani kutega mingo, Timu ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ilipokea mchongo kuwa kuna timbwili kwenye gesti moja maeneo ya Buguruni, Dar ambapo walifika eneo la tukio na kushuhudia kasheshe hilo la aina yake. Ndugu wa mume waliyefumania wakimdhibiti baba mwenye nyumba huyo.  OFM ilimshuhudia mzee huyo akichomolewa kutoka chumbani huku damu zikimvuja baada ya kula kichapo kutoka kwa jamaa na ndugu wa mwanaume aliyedai kuwa jamaa huyo alikuwa anamsumbua mkewe. Mke aliyekuwa akisumbuliwa, na

Dk Salim afichua siri ya JK na Tume ya Warioba

Image
Dar es Salaam. Waziri Mkuu Mstaafu, Dk Salim Ahmed Salim amesema hakutarajia kusikia kauli za Rais Jakaya Kikwete alizozitoa bungeni kukosoa Rasimu Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa sababu walikuwa wanampa taarifa kwa kila hatua waliyokuwa wanafikia kabla ya kutoa rasimu hiyo.                Dk Salim alitoa kauli hiyo katika mahojiano maalumu na gazeti hili nyumbani kwake Masaki, Dar es Salaam wiki iliyopita. “Hatukutarajia kama hali ingefikia hatua iliyofikia,” alisema Dk Salim na kuongeza: “Lakini Rais ana uamuzi wake na anazingatia mambo mengine mengi.” Akilihutubia Bunge maalumu la Katiba Machi 21, mwaka huu Rais Kikwete aligusia mambo saba ya msingi yaliyomo katika Rasimu ya Katiba na kutaka yatazamwe kwa kina, huku akibainisha kuwa mengine hayawezekani kutekelezeka. Miongoni mwa mambo hayo ni muundo wa Serikali. Alipinga waziwazi pendekezo la serikali tatu lililopendekezwa na Tume na kuegemea katika muundo wa serikali mbili na idadi ya watu walioupendekeza

RED CARPET YA TUZO ZA BET 2014

Image
Diamond Platnumz akihojiwa na Karrueche Tran ambaye ni mpenzi wa Chris Brown kwenye Red Carpet. Amber Rose. T.I. Gabrielle Union. Ne-Yo akipozi kwenye Red Carpet. Ashanti. Nelly. Claudia Jordan. John Legend. Eva Marcille. Lionel Richie. Jennifer Freeman

BOKO HARAM WASHAMBULIWA NA NYOKA WA AJABU NA NYUKI, WAKIMBIA PORINI

Image
Wanajeshi wa Boko Haram wanaofanya mashambulizi na kuua raia wasio na hatia huko Nigeria linaelezwa kuanza kukimbia msitu baada ya nyoka wenye sumu kali na nyuki kuwashambulia. Habari hizi zilielezwa na mtuhumiwa mmoja aliyekamatwa na kuthibitisha kuwa ni mmoja wa member wa kundi la Boko Haram na alieleza kuwa hivi sasa kundi hilo limelazimika kuhama msitu na linaelekea maeneo ya mpaka wa Nigeria na Cameroon baada ya wanajeshi wake wa ngazi za juu kushambuliwa na nyoka na kupoteza maisha. Kumezuka hisia za kiimani kuwa Boko Haram wanaadhibiwa na mizimu ya watu waliokuwa waliowauwa kinyama.Jeshi la Nigeria limeshafanya juhudi za kuwaondoa msituni lakini imeshindwa na hadi sasa kundi hilo linawashikilia wasichana zaidi ya 260 na bado linaendelea kushambulia Nigeria kwa mabomu ya kutegwa.

Kutana na mtaalamu Rob Ferrel kutoka Rob the Original Barbershop San Antonio ambaye hunyoa wateja kwa taswira za wachezaji wawapendao

Image
Wakati mashindano ya Kombe la Dunia yakishika kasi nchini Brazil, kimetokea kituko cha aina yake hasa kwa mashabiki wa soka nchini Marekani ambapo Salon moja mjini San Antonio inatoa ofa ya kunyoa nywele kwa michoro ya wachezaji mbalimbali nyota wanaotamba katika fainali hizo.  Katika wiki za hivi karibuni Rob Ferrel, mmilikiwa wa Rob the Original Barbershop, aliwanya watu kwa picha ya sura za nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo, mlinda mlango wa Marekani Tim Howard na Guillermo Ochoa kama sehemu ya ubunifu wake wa kunyoa.  Licha ya timu ya Ronaldo kuondolewa kwenye hatua ya makundi, walinda mlango wa Marekani Howard na Mexico Ochoa watakuwepo kwenye hatua ya mtoano. Vipi kuhusu hii? Rob Ferrel akimnyoa mteja kwa sura ya mlinda mlango wa Marekani Tim Howard Amemaliza: Tim Howard na bendera ya Marekani Miaka minane iliyopita Ferrel alikuwa anafanya kazi kwenye barbershop moja mjini Texas wakati ambapo kijana huyo alipoanza kuwau

ANGALIA PICHA JINSI WANACHAMA WA SIMBA WALIVYOPIGA KURA LEO KUCHAGUA VIONGOZI WAPYA

Image
Wanachama wa Simba wakiwa katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Viongozi wa Klabu ya Simba katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo. (Picha na Francis Dande) Wagombea wa nafasi ya Urais katika Klabu ya Simba, Evans Aveva (katikati) na Andrew Tupa na wakipiga kura wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa klabu hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam.  Hassan Dalali akipiga kura.  Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu na Rais wa Simba anayemaliza muda wake, Ismail Aden Rage wakipiga kura.  Rais wa Simba aliyemaliza muda wake, Ismail Aden Rage akiagana na mgombea wa Urais wa Simba, Evans Aveva (katikati).  Wagombea wakitafakari.    Wanachama wakihakiki kadi zao. Mgombea wa Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba, Godfrey Nyange 'Kaburu' akizungumza na baadhi ya wanachama kabla ya uchaguzi. Mgombea akiomba kura......Tukiwezeshwa tunaweza.  Mgombea akijinadi.  Mgombea wa nafasi ya Kamati ya Ute